Showing posts with label Ufunguzi wa Kituo. Show all posts
Showing posts with label Ufunguzi wa Kituo. Show all posts

Friday, 15 March 2013

Baadhi ya Picha za Ufunguzi wa Kituo cha Canaan Children Center

 Askofu Mkuu wa Jimbo  la Arusha Mhashamu Josaphat L. Lebulu, 
akifungua rasmi kituo cha Malezi ta watoto cha Canaan Children Centre

Tuesday, 12 March 2013

Taarifa ya Ufunguzi wa Kituo cha Watoto cha KANAANI – Kisongo Tar. 17 Feb 2013



Kituo cha Watoto cha Kanaani – Kisongo, kilifunguliwa rasmi na Mhashamu Baba Askofu Mkuu Josaphat Lebulu kwa Misa Takatifu ya kukibariki siku ya Jumapili Tar. 17 Februari 2013. Misa hii ambayo iliadhimishwa na Mhashamu Baba Askofu Mkuu akishirikiana na mapadre  12 ilihudhuriwa na wana Familia ya Mungu ya Arusha zaidi ya 600, pamoja na marafiki wa kituo kutoka Ujerumani (Partnership for Africa), na viongozi wa serikali wakiwakilishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa na Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa.